MKUU WA MAJESHI YA ISRAEL, HERZI HALEVY, ALIKIRI "KUFELI KWA JESHI MNAMO OKTOBA 7 NA KUSHINDWA VITA NA HAMAS HUKO GAZA
Mkuu wa majeshi wa Israeli, Herzi Halevy, anakiri kushindwa kwa "jeshi" mnamo Oktoba 7, na Waziri wa Fedha katika serikali ya uvamizi, Bezalel Smotrich, anawashambulia Mkuu wa majeshi, akisema kwamba "ilileta moja ya maafa makubwa zaidi kwa israel. Mkuu wa majeshi wa israel, Herzi Halevy, alikiri "kufeli kwa jeshi mnamo Oktoba 7," akisema: "Jukumu liko kwetu." Halevy aliongeza, katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, kwamba "Israel ina safari ndefu kufikia malengo yake ya vita," akibainisha kuwa "kusimamisha uteuzi kwa uongozi wa jeshi kutaathiri kazi yake." Mkuu wa Majeshi pia alieleza "utayari wa Jeshi kupanua operesheni ya kijeshi kwa mujibu wa maamuzi ya ngazi ya kisiasa." Vyombo vya habari vya Israel viliripoti kwamba Halevy atafanya mchakato mkubwa wa uteuzi katika "Jeshi" kesho katika cheo cha kanali, kwani angewateua maafisa wapya 52, "ikiwa ni pamoja na nyadhifa mbili zinazochuku...